Header Ads

Header ADS

MAMBO 6 YA KUFANYA KABLA HUJAMALIZA MWAKA:JIFUNZE MBINU ZITAKAZOKUSAIDIA KUANZA MWAKA KIVINGINE.

Tuanze kwa kujifunza,baadhi ya vitu: Tony Robins aliwahi kusema "If you do what you have always done,you will get what you have always gotten" (Kama utaendelea kufanya,unavyofanya kila siku,utaendelea kupata matokeo unayoyapata kila siku) Watu wengi wanataka kupata matokeo makubwa lakini hawako tayari kufanya mambo makubwa. Naombeni niendelee kunukuu: *Wanataka kuongeza kipato bila kuongeza vyanzo vipya vya kuingiza kipato. *Wanataka kuwa waimbaji wazuri bila kujinoa zaidi. *Wanataka kuwa waandishi bora bila kujiboresha. *Wanataka fursa mpya,bila kuzitafuta. *Wafanya biashara wanataka kuongeza mauzo kwa kutumia mbinu zilezile wanazozitumia kila siku. *Wakulima nao wanataka kuongeza mavuno bila kubadili namna wanavyolima siku zote. Kupata matokeo mapya bila kubadili namna unavyofanya,ni kujidanganya haiwezekani na kamwe haitowezekana.Dunia huwa inampatia mtu matokeo sawasawa na kile anachokifanya. Mara nyingi hujikuta tukiwa,na mipango au malengo mengi huku tukishindwa kuitimiza.Hii hutokana na namna utavyoishi,huwa tunakuwa sawa na tulivyokuwa jana. Ili mipango au malengo yaweza kutimia unahitaji mienendo tofauti na ile tulivyokuwa nayo mwanzoni.Tunahitaji kuwa na fikra za kitofauti na zile tulizokuwa nazo mwanzoni. Kabla hatujamaliza mwaka,inabidi tujifunze vitu vipya vitakavyotusaidia kutimiza mipango yetu.Tunahitaji kujifunza vitu ili tusiwe watu kama wa jana au kipindi cha nyuma. MAMBO YA KUFANYA KABLA YA KUMALIZA MWAKA: 1.Kuwa na Mungu karibu zaidi. Tunahitaji kumshukuru Mungu,kwa kila jambo liwe zuri au baya.Kipindi hichi,tunapaswa kukumbuka namna Mungu alivyotulinda na kutupigania.Kipindi hichi,mambo mengi huwa yanayotokea hivyo tunamuhitaji Mungu,ili tuweze kuvuka mwaka mwingine. Ni muda wa kuikabidhi mipango yako uliyoweza kuitimiza na ambayo hujaitimiza yote kwa Mungu:Bila yeye,sisi si kitu.Hiki ni kipindi cha utulivu,unachopaswa kuwa karibu na Mungu.Huu ni wakati tunahitaji kuomba ulinzi na nguvu za Mungu. 2.Pata mda wa kwako binafsi. Ukweli ni kuwa,mda huu wa mwisho wa mwaka unahitaji kupata mda wa kuwa mwenyewe,wewe na akili yako.Mara nyingi huwa tunakuwa na watu,tunapitia mengi na wakati mwingine tunakosa mda wa kujiliwaza na kutuliza akili zetu. Tunahitaji mda wa peke yetu,ili tujikumbushe ni wapi tunatoka,na wapi tunahitaji kwenda.Kwa sababu,usipojua wapi unatoka na wapi unahitaji kwenda,huwa ni rahisi sana kupotea njiani. Hii husababisha watu kuahirisha baadhi ya mipango au malengo waliyojiwekea.Kukosa shauku la kusonga mbele,huku wakikatishwa tamaa na mazingira,ndugu,marafiki au jamaa. Ikiwa utapata mda wa peke yako kwa siku,itakuwa ni wakati mzuri zaidi wa kutambua,wapi ulianguka,wapi unahitaji nguvu zaidi na wapi vitu vilienda vibaya.Hayo yote yatakuandaa vyema kwa miaka ijayo,ili usiweze rudia mambo yale yale. "Nakumbuka kuna kipindi nilikuwa ninapanga mipango mingi na mizuri mwanzoni mwa mwaka,na wakati mwingine nikijiahidi kutokuwa na mienendo niliyokuwa nayo kipindi kilichopita lakini mambo yalikuwa tofauti.Nilijikuta baada ya muda narudi na mambo yaliyopita.Hivyo nikawa mtu wa kujilaumu kila wakati". Baadye nikagundua pia kuna wakati ubongo unahitaji kupumzika ukiwa mwenyewe.Inaweza ikawa nyumbani,hotelini,ufukweni,au eneo lisilo na watu,ili upate mda wa kujitafakari. "Natoka wapi,nafanya nini,naenda wapi"Hakikisha ni lengo lako kuwa kama mwanzoni. 3.Kupanga mipango mipya. Usiogope kuwa na mipango.Mipango mikubwa hukupa nguvu na shauku la kuifikia.UKIWA NA MIPANGO MIKUBWA,BASI KUWA MKUBWA. Ili uweze kupanga mipango inayotimizika,inakupasa kufahamu: *Unapaswa kujikumbusha mikakati yako ya nyuma. *Malengo gani yanayohitaji marekebisho. *Ni wapi ulikwama na unahitajika nguvu za ziada. *Ni nini kilikufanya ukashindwa? *Ni mbinu gani wapinzani wako huzitumia kukuzidi? Hayo yote yatakusaidia kufahamu ni nini unachokilenga haswa. Kutoka kwenye kitabu cha THE POWER OF SELF DISCIPLINE,mwandishi anatupa mbinu zitakazotusaidia kufikia mipango au malengo tuliyonayo. (i)Tafakari lengo au mipango yako. Mwandishi anaelezea,kuwa baada ya kuandika malengo yako kwenye daftari,inapaswa uweze kutafakari malengo yako,ikiwa ni kweli unaweza kutimiza malengo uliyojiwekea ndani ya mda uliopanga. Mfano:Nimepanga kujenga nyumba ndani ya mwaka ujao.swali la kijiuliza ni:Je,naweza kujenga nyumba ndani ya mda niliojiwekea?Je naweza kumudu gharama za ujenzi? Fahamu kuwa kuna mipango mingine mikubwa huwa inaitaji mda,ili tuweze kuitimiza.Hivyo tuwe makini na machaguzi ya mipango tunayohitaji kuitimiza. (ii)Weka mikakati juu ya malengo uliyonayo. Hapa Mwandishi anaelezea kuwa lengo peke yake,si lengo ikiwa hamna mikakati inayohitajika kufikia lengo hilo.Kuwa na mikakati hurahisisha sana kufikia lengo kuu. Huwezi kutimiza malengo au mipango uliyonayo ikiwa huna mikakati.Mikakati,ni hatua ndogo zitakazokusaidia kwenye malengo yako. Mfano:Nna lengo la kuweka kiasi cha shilingi 200,000 kwa mwezi.Hivyo baadhi ya mikakati unayopaswa kujiwekea ni pamoja na:Kuwa na vyanzo mbalimbali kuongeza kipato,kiasi unachopaswa kuhifadhi kila siku,ili kufikia lengo kuu,kupunguza gharama za matumizi ya kila siku. Hiyo ni moja kati ya mikakati unayopaswa kujijengea,ili kufikia lengo kuu. 4.Tengeneza mtandao na watu wenye umuhimu. Ikiwa wote tumeumbwa na Mungu,basi kila mtu ana umuhimu kwenye maisha tunayoishi.Jambo la mihimu,ni watu wapo wengi lakini tunapaswa kuwa na watu watakaotusaidia kufikia kule tunapohitaji kwenda.Inapaswa tuwe na watu watakaotufanya tuzidi kwenda mbele zaidi, kujuana na watu wengisio tatizo,tatizo ni ikiwa wanakusaidia kufikia unapoenda. Tunapaswa kuwa na watu watakaotukumbusha,mara kwa mara juu ya tunapoenda.Ikiwezekana familia au watu wanaotupenda.Baadhi ya sehemu,tunahitaji uwepo wa watu wengine ili tufikie kule tunapopahitaji. Mfano,Mwanafunzi anapaswsa kujenga mtandao na wanafunzi wengine.Mtandao utakaomsaidia kitaaluma,mtandao utakaomsaidia kufikia malengo yake kitaaluma. Endapo,upo nyumbani na hujui nini cha kufanya,unaweza uliza wazazi wako au marafiki kuhusu kazi ndogondogo ambazo unaweza kujiingizia kipato.Hakikisha mwakani,unajenga mtandao wa watu wa muhimu watakaokusaidia kufikia malengo yako,na kule unakohitaji kwenda. 5.Jambo lolote unalolianzisha,hakikisha unalikamilisha. Kuhusiana na safari ya kufikia mipango tuliyonayo,kuna vitu vinavyoturudisha nyuma katiks kufikia tunapoenda. Mfano:Je ni mipango gani uliyoacha kuifanya,kutokana na changamoto au vikwazo ulivyopitia? Hivyo siyo sababu ya mtu kukata tamaa.Mda mwingine kuliko kuahirisha baadhi ya mipango tunahitaji kupata mda wa kupumzika.Pumzika kisha rudi kuendelea na kazi. Njia ya kufikia tunapoenda huwa na vikwazo vingi,vingine hutoka kwa watu tuliowapenda na kuwaamini.Ni bora,kuweka makubaliano kuwa kwa hali yoyote ile basi ukamilishe jambo ulilopanga kulifanya. 6.Usiache kujipongeza. Kujipongeza huchochea morari na mwanzo mpya hivyo,ni vyema endapo tutajiwekea mipango au tukaweza kukamilisha jambo fulani hata liwe dogo kiasi gani.Tusiache kujipongeza. CHUKUA HATUA SASA. Usiache kuhudhuria darasa letu la uchsmbuzi wa vitabu.Gharama ya shilngi 1000 kwa mwezi vitabu vitakavyokusaidia katika mmaisha yako.Utachangia gharama hiyo kupitia namba 0746650818 Jina UPENDO ERNEST,na utatuma uthibitisho wako kupitia whatsapp na utaunganishwa kwenye group. *Unaweza pia kununua kitabu cha OPEN THE DOORS OF SUCCESS IN YOUR ACADEMICS,ukapata na kingine burreh kabisa. Maoni yako ni muhimu sana kwetu.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.