Tabia 4 zinazowafanya maskini wengi wazidi kuwa maskini:Leta mabadiliko.
YALIYOMO
>Utangulizi
>Mifano kutoka kwa wanafalsafa wa zamani.
>Tabia znazowafanya masikini walizikuendelea kuwa masikini.
>Njia mbalimbali za kujiondoa kwenye duara la umasikini.
1.Utangulizi.
Umasikini ni nini?
*Uchumi au kiwango cha watu wanavyoishi duniani kote huwa vnatofautiana,wengine ni matajiri,wenye vipato vya kawaida na masikini.
Hata na hvyo,utafiti unaonesha watu wengi walio maskini huwa na matumizi ya shilingi 2000 kushuka chini kwa siku.Ikiwa kwenye biashara zao,wao huanzia kupata faida ya shilingi 2000 na kuendelea.
Pia inaonesha kuwa Zaidi ya watu milioni 700 wanaishi kwenye hali ya umasikini duniani kote.
Ingawaje wote tumezungukwa na watu matajiri na uwezo kutuzidi sisi.Idadi hii ya watu ni kubwa mno.
Ndipo mwanafalsafa na mchumi Ragnar Nurkes akaja na wazo au mada kuhusiana na “Viscous circle of poverty”. Lakini pia alisema kuwa “Poor is poor because is poor”
Akiwa na maana masikini ni masikini kutokana na umasikini.Hivyo ni vigumu sana kwa masikni kutoka kwenye duara la umaskini.
Viscous circle of poverty au niliite DUARA LA UMASIKINI,inaonesha kuwa umasikini ni sababu ya umasikini.
Mtu masikini,ili aweze kulipa madeni yake atakopa fedha Zaidi kwa ajili ya kulipia madeni,hvyo basi deni lake litaongezeka.
Nikiwa na maana madeni yake yatakuwa mengi.
Maskini huyo hurithisha madeni kwa kizazi chake kinachokuja:ambapo na watoto wake watakuwa kwenye mzunguko wa duara la madeni na umaskini.
Nurkes alimaliza kwa kusema masikini hubaki kuwa maskini na hurithisha umasikni kwenda kizazi kingine. Kwa hali yoyote,kujenga utajiri na kujiondoa katika duara la umasikini inawezekana ikawa changamoto,lakini ni jambo linalowezekana.
Nurkes alifanikiwa kutoa chanzo cha watu kuzidi kuwa kwenye duara la umaskini,wakati hakutoa mapendekezo ya nini cha kufanya ili kujitoa katika duara la umasikini.
Tuanze.
Sababu 4 zinazowafanya masikini wazidi kuwa masikini.
Hivyo nitachambua sababu nilizojifunza znazoendana na sababu zake.
1.Imani.
“Under all that we think,lives all we believe,like the ultimate veil of our spirits” Antonio Machado.
Nitolee mfano wa mwandishi.Mzee mmoja mlevi,teja wa madawa ya kulevya na mkatili,alihukumiwa kifo kwa kosa la mauaji ya mhudumu wa bar.
Mzee huyu alikuwa na watoto wawili wamepishana miezi 11.Mmoja kati yao ni teja wa madawa ya kulevya,mlevi na mkatili kama baba yake.
Mtoto mwingine ana utofauti,kaoa na anandoa yenye furaha.Sio mlevi,mkatili au teja wa madawa ya kulevya.Kiafya na kiakili yupo vizuri.
Inawezekanaje vijana hawa waliozaliwa pamoja na kuishi eneo moja wakawa na tabia tofauti?
Vijana wote wawili waliulizwa,kila mtu kivyake.Lakini cha ajabu majibu yao yalikuwa sawa kwamba “wote wamelelewa na baba”
Mwandishi anazungumzia namna tunavyolazimishwa na kuamini kuwa mazingira tuliyotokea ndiyo yametufanya tuwe tulivyo leo.
Sio matukio tuliyoyapitia ndio yametutanya tuwe hivi tulivyo leo,lakini ni namna tunavyoamini kutokana na mazingira tuliyopitia.
Mfano,unaweza ukawa umetokea kwenye familia masikini,ingawaje una ndugu,jamaa,kaka au dada ambaye umezaliwa nae na sio masikini kama wewe.
Matatizo yaliyompata na yaliyokupata,mkiwa nyumbani ni sawa.utofauti unakuja ni Imani gani unayoijenga kutokana na hilo tatizo.
Asilimia kubwa ya masikini huamini kuwa wametokea katika familia maskini na watakufa maskini.
Imani kama hiyo husababisha hata kizazi kinachofuata kuamini kuwa wao pia ni maskini. Hivyo basi unaona kuwa,sio mazingira wala matukio tuliyoyapitia ndio yanatufanya tuwe hivi tulivyo leo,ila ni taswira tunayojijengea ndio hutufanya tuamini na kutufanya tuwe hivi tulivyo leo.
Familia nyingi tunazotokea wazazi hutuaminisha kuwa umerithi tabia za mtu Fulani,labda babu,bibi na wengineo. Taswira utakayojiwekea,ndio haswa hukufanya uamini kuwa upo hivyo.
Ni vyema ikiwa tutabadilisha,namna tunavyoamini baadhi ya vitu.
2.Uhifadhi duni.
Changamoto ingine imeelekezwa kwenye uhifadhi duni kutokana na kipato kuwa kidogo.
Masikini huwa wanauwezo mdogo wa kuzalisha kipato au mapato,hivyo kiwango chake cha uhifadhi wa fedha na chenyewe ni kidogo.
Ili maskini aweze kutoka kwenye duara la umaskini,suala la kuwa na uwezo wa kuhifadhi fedha ni muhimu.
Uhifadhi wa fedha,unahitaji nidhamu binafsi na uvumilivu.
Ukosefu wa uvumilivu,hufanya ndoto,mipango na misimamo ya baadhi ya watu kupotea.
3.Uwekezaji duni.
Kuwekeza inahitaji uwe na ufahamu Zaidi wa vitu vilivyokuzunguka.
Ili uweze kuwekeza inapaswa kujijengea Imani kuwa huduma unayoitoa ni bora Zaidi kuliko watu wengine. Masikini huamini hawawezi kufanya uwekezaji na kufanikiwa,ikiwa amepitia changamoto na matatizo yaliyomfanya aamini kuwa hawezi kuwekeza.
Kuwa mwekezaji inapaswa kuhakikisha umezungukwa na taarifa au watu sahihi watakaokusaidia kufikia unapopahitaji.
Masikini huchukia kujifunza haswa kwa ndugu,au jamaa na watu waliomzidi kipato au maisha.
Hivyo ni ngumu kupata changamoto mpya zitakazomsaidia kufikia anapopalenga.
Ikiwa umezungukwa na jamii ya watu wavivu na hawana mawazo chanya,utafuata mkondo huo. Jiwekee malengo ya kujifunza mengi kwenye uwekezaji.
4.Uzalishaji duni.
Uzalishaji,ni uwezo wa kutoa kitu au matokeo ya kitu.
Kutokana na maskini kukosa kipato cha kutosha,hata hufikiri hawawezi kuzalisha kitu kitakachoweza kuleta manufaa kwenye jamii.
Wamewekwa kwenye duara la umaskini wa fikra,ambalo ni vigumu kulivunja.
Hujiona hawawezi kufanya kitu au jambo lolote.Hivyo,uzalishaji hutokana na maamuzi atakayoyafanya mtu. Tunashindwa kutambua,kuwa kila maamuzi tunayoyafanya siku zote,hujenga hatima yetu.
Mafanikio au kufeli kwenye maisha hutokana na maamuzi yetu ya kila siku.Amini unaweza . Uwezo wa masikini kufanya uzalishaji ni duni,kwani hawezi kutumia kitu alichonacho kupata kitu kingine. Amefungwa kwenye duara ambalo linahitaji juhudi kulivunja.
Umejifunza kitu? Sehemu inayokuja tutajifunza namna ya kutoka kwenye duara hilo la umasikni. Unaweza kujiunga na kujisajili kwenye darasa la UCHAMBUZI WA VITABU,kwa gharama ya shilingi 1000(mwezi mzima).Lipia kupitia namba 0746650818 Jina UPENDO KITUNDU.
Utaendelea kupata somo lijalo.Na kujifunza vitabu vitakavyokusaidia. Namna ya kutoka kwenye duara la umaskini.
1.Jielimishe mwenyewe.
Nakumbuka mwalimu wangu alishawahi kusema “Huwezi kusaidia familia yako,ikiwa hutaanza kujisaidia wewe kwanza” Inakupasa kujielimisha na kujitoa kwenye eneo la duara la umaskini,kisha utaweza kuivusha na familia yako. Familia zenye wasomi au watu waliosoma ni vigumu sana kuikuta maskini.
Elimu tu huwa ni msingi na ujuzi anaoupata mtu utakaomsaidia atoke eneo alilopo kwenda eneo linguine,kupitia ujuzi alionao. Elimu inaweza isiwe ya kalamu na daftari pekee.
Jaribu kutafakari maeneo ya karibu na wewe au watu wako ambao hawana elimu na maisha wanayoishi. Ikiwa mtu atajitambua na kujielimisha kwenye kitu ambacho anahisi kitamletea mafanikio,basi anauwezekano wa kusaidia na wenzake wanaomzunguka.
Jambo la muhimu,ni ikiwa tutaamua kujikumbusha na kuwakumbusha watu au wanafunzi kuwa wanajielimisha ili waweze kujisaidia wenyewe na jamii inayowazunguka.
Swali la kujiuliza:Nawezaje kujielimisha kutoka hapa nilipo?
Unaweza kujielimisha kupitia semina mbalimbali,kozi mbalimbali za mtandaoni zenye manufaa kwako,lakini pia kusoma vitabu,kupitia darasa letu la Uchambuzi wa vitabu.
Maskini yupo radhi kujitolea hela yake akanywa pombe au kuichezea,bila kujifunza kitu kipya kitakachomsaidia maishani.
Ndio maana tumerahisisha na kuja na kampeni ya UCHAMBUZI WA VITABU mbalimbali vya kutusaidia maishani. Gharama ya kuwa kwenye darasa la UCHAMBUZI WA VITABU ni 1000Tsh kwa mwezi.
Malipo yote yanalipwa kupitia namba 0746650818 Jina UPENDO KITUNDU.Utatumiwa link ya group na utaweza kujielimisha taratibu,ili wote tutoke tulipo.
Chaguo ni lako leo,unaweza ukaamua kwenda mbele kwa kujielimisha na vitu vipya kila siku,kuliko kukaa siku nzima.
Wakati ambao hujajielimisha na kitu Fulani,itakuwa ni vigumu sana kulikimbia duara la umaskini. Hakikisha kuwa unachojielimisha kinaleta maendeleo kwa wanaokuzunguka.
2.Usiogope kutoka hapo ulipo.
Katika safari ya mafanikio yoyote yale,ni lazima baadhi ya watu wataondoka kwenye maisha yako ili uweze kutoka kwenye duara la umaskini.
Kama unaona hujawahi kubadilika,au watu waliokuzunguka hawajabadilika basi fahamu kuwa hujawahi kupiga hatua kimaendeleo. Kuna nyakati ambazo utasaidiwa na watu,tofauti na uliowazoea. Muda mwingine ni kukubali na kuendelea na mambo yako.
3.Muulize mtu unayemwamini.
Mtu ambaye utaweza kumwelezea hali yako,na kumwomba ushauri wa jinsi utakavyoweza kujikwamua kutoka sehemu uliyopo.
Hakikisha mtu huyo anafahamu kitu walau,cha kukuhusu na hali unayoipitia au anaijua hali yako. Kuna baadhi ya watu hupenda kutumia hali zetu kutuumiza na kututangaza mabaya kwa watu.Mara nyingi huondoa kujiamini.
Mtu anayetamani kuona ukifanikiwa na kufikia eneo Fulani. Mrejesho wako ni wa muhimu kwangu. Asante na Mungu Awabariki.

Hakuna maoni