Header Ads

Header ADS

Makosa 6 yanayotuzuia kufanya mambo katika viwango vikubwa:Jifunze,kisha fikia malengo yako kwa kujiamini.

1.Kila kitu sawa.







Nakumbuka kipindi nasoma,nilikuwa na mipango mingi.Siku hiyo,usiku baada ya watu kulala nilichukua daftari langu na kuandika baadhi ya mipango itakayonisaidia nfaulu vzuri sana darasani.








Mipango ilikuwa mingi,lakini kwa hali halisi kuwa na mipango mingi haimaanishi kuwa tayari wewe ni mshindi au umeshafanikiwa tayari.

















Huwa tunaangalia ni namna gani ulivyoweza kutimiza kila mpango kwa usawa. Nikiwa na maana,kuwa mara nyingi huwa tunakuwa bize na imara kwenye mambo yaliyotupeleka kwenye mipango yetu,huku tunaamini kuwa bado tutafanikiwa.












Moja kati ya kosa tunalolifanya ni,kupita siku bila kufanya walau kitu kidogo kwa ajili ya ndoto na mipango yetu. Waandishi wa kitabu cha ONE THING,wanaeleza kuwa unaweza ukapanga mipango mingi kwenye kila kitu maishani,lakini wapi haswa unahitaji kwenda. Katika mengi tunayoyataka,tunajikuta tumetimiza machache. Ikiwa tunahitaji matokeo makubwa Zaidi ya kile tunachokifanya,basi mipango yetu inapaswa kuwa na vitendo au jitihada zetu. Haijalishi ni aina gani ya lengo au mpango unaohitaji uutimize. Hivyo kosa,tunalolifanya ni kufikiri kuwa jitihada itakuwa sawa kwenye kila mpango. Ni vizuri,kuweka mipango maishani lakini bila kuwa watendaji huwa hamna tunachokifanya.






Swali la kijiuliza: Ni mipango gani ulikuwa nayo,Je uliweza kuitimiza kwa jitihada sawa? Kila tunapokuwa na mipango maishani,Mwandishi anatuhasa kuwa tuhakikisha tunakamilisha mpango huo. Yaani KILA ULILOLIANZISHA,HAKIKISHA UNALIKAMILISHA. Katika kila mipango tunayojiwekea maishani,mar azote huwa kuna mpango ambao ni wa muhimu Zaidi kuutimiza kuliko mipango mingine. Inawezekana,mipango hiyo mingine ikawa sio lazima kuifanya kwa muda huo,ila hakikisha unaanza na mipango ya muhimu Zaidi.










2.Kufanya Kazi Nyingi.






Mwandishi anazungumzia kuwa kufanya kazi nyingi ni uongo. Ukijaribu kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja,unaweza usiweze kabisa kuyafanya mambo hayo au usiyafanye mambo kwa ufanisi(vizuri). Katika kitabu cha NIDHAMU BINAFSI,mwandishi anatoa hamasa kuhusu kufanya jambo moja kwa wakati,kisha kuhamia jambo lingine. Shida huwa sio kwamba hatuna mda wa kuyafanya mambo hayo,lakini huwa tunajaribu kuyafanya mambo mengi kwa wakati mdogo. Fahamu kuwa huwezi kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja,lakini huwezi kuwa makini kwenye kuyafanya mambo(mipango) miwili kwa wakati mmoja. Utafiti unaonesha kuwa,unapoteza ufanisi unapofanya mambo mawili kwa wakati. Mfano,unaandika ripoti huku unajibu meseji kwenye simu.




3.Kukosa nidhamu binafsi. Suala la mafanikio,kwenye kila tunachokifanya nidhamu binafsi ni moja kati ya nguzo muhimu. Ukiwa na nidhamu binafsi,unajifunza mwenyewe namna ya kuwa katika baadhi ya vitu. Unaweza kuwa mwenye mafanikio,lakini huna nidhamu binafsi.Hii ni kwa sababu mafanikio ni suala la kufanya jambo sahihi,sio kuwa sahihi.




Ukifikiria sana utagundua kuwa,watu hupenda kufanya mambo bila kukosea,yaani wawe sahihi kwenye kila wanachokifanya. Siku zote mafanikio huenda sambamba na kufeli au kuanguka.Ikiwa hupendi kufeli,kisha sahau kuhusu kufanikiwa. Nidhamu binafsi,hutusaidia kupunguza baadhi ya makosa tunayoyafanya kila siku.Makosa ya kuepukika. Ili uweze kufanikiwa,chagua tabia sahihi au mienendo unayohisi ukiwa nayo utafanikiwa. Ukimaliza,anza kushughulikia jambo moja au mpango mmoja,kisha nenda mwingine. Kujenga tabia au mienendo mipya ya mafanikio huchukua kuanzia wiki 54 na kuendelea. Ukiwa unajenga nidhamu binafsi,hakikisha unaendelea kutimiza mipango mingine maishani.





4.Nguvu ya mapenzi iko daima. Kivipi? Tunavyozidi kutumia fikra zetu,ndivyo nguvu ya kifikra hupungua. Wakati wote,huwa tunafanya mambo ya muhimu tukiwa na mapenzi na jambo hilo. Jinsi mda unavyozidi kwenda,shauku na mapenzi ya kufanya mipango au baadhi ya mipango hupungua. Ikiwa unahitaji kupata matokeo makubwa Zaidi ya kila ulichopanga kukifanya.Hakikisha unafanya mambo yako yote ya muhimu,haraka na kwa wakati kabla ya nguvu,mapenzi au shauku ya kufanya mipango hiyo haijapungua.









5.Kuishi maisha ya usawa. Mwandishi anazungumzia kuwa,haijalishi namna gani unajaribu kufanya baadhi ya mipango,mwisho wa siku baadhi ya mipango haitakuwa imekamilika. Sio lazima baadhi ya mipango iwe imekamilika baadhi ya vitu. Ukiwa unapanga kubaliana na hali kuwa,kuna baadhi ya vitu vitaenda ndivyo sivyo. Kutimiza mpango au jambo,kwa viwango vingine tunapaswa kuhakikisha tunafanya mambo ya msingi na muhimu kwanza. Kuna wakati utahitaji kuweka sawa,mambo ya kikazi,mipango,na kifamilia. Kipe kila kitu,mda wake.Ndipo utaweza kufanya mambo katika viwango vya kitofauti.









6.Ukubwa ni vibaya. Ikiwa utakubali mwenyewe mambo makubwa,basi utaonekana mtu wa kitofauti. Watu wasioona mambo makubwa yakitokea kwenye mipango yangu,huwa ni vigumu sana kuendelea pindi mambo yakienda mrama. Jenga ndoto kubwa,usiogope kuona makubwa ndani yako. Kuna baadhi ya nyakati,tunakatishwa tamaa na watu wa karibu.Hivyo tunashindwa kujiona tena,tukifanya mambo ya viwango vya juu Zaidi na vile vya mwanzoni. Jiamini,na jaribu kufanya kitu kipya kila siku. Kumbuka unachokifanya leo,kinakuonesha wewe ni nani kesho.Bado hujachelewa unaweza kufanya makubwa kutoka hapo ulipo.



Usisahau kujiunga na wengine,DARASA LA UCHAMBUZI WA VITABU,vitakavyokusaidia kutoka eneo moja hadi lingine. Gharama ni shilingi 1000(mwezi mzima) kupitia namba 0746650818 Jina UPENDO KITUNDU.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.