Header Ads

Header ADS

Mbinu 9 za kuwa mwanafunzi bora kitaaluma:ZINAFANYWA NA WATU WANAOFAULU ZAIDI KITAALUMA.

Ukweli ni kwamba,kila mtu ana akili,hakuna mtu ambaye hajapewa utashi wa kufikiri na kufanya mambo makubwa.Tofauti inakuja pale ambapo tunazitumia akili zetu. Ushawahi kujiuliza,huwa una akili kiasi gani?Mungu alituumba kila mtu ana akili,lakini kwenye suala la matumizi ya akili zetu ndipo sehemu huwa tunatofautiana.Kuwa mwanafunzi bora kitaaluma ni jambo ambalo naweza kusema linawezakana endapo kama wewe mwenyewe utaamua kuipigania nafasi hiyo.Nakumbuka kipindi nasoma,mwanzoni nilikuwa nafeli sana,nilikuwa karibu na watu wanaofanya vizuri lakini kila wakinifundisha shda bado kwangu,kwani nilikuwa sielewi. Muda mwingine nilikuwa nikikaa mwenyewe mahali,nikijitafakari kuhusiana na namna ambayo itanifanya nirudi na kufanya vizuri.Huwa mara nyingi,tunaposhindwa kufaulu kama vile tunavyohitaji kujiamini huwa kunapungua,pindi ambapo watu wa familia yako na jamii ikiamini unaweza kufanya vizuri. Kwa kipindi hcho nilijipa mda,nikaanza kuangalia vidio za YOUTUBE kuhusiana na namna mtu anaweza kuwa mwanafunzi kitaaluma na akaweza kutoka kwenye kupata F hadi A.Nilikuwa nikimwomba mama yangu simu,naangalia vidio nikiwa na daftari kwa ajili ya kuandika mambo ya muhimu.Nilisoma vitabu vingi sana vya namna ya mtu kufaulu.Namna bora ya kuongeza kumbukumbu na kukumbuka kila unachokisoma,kila nilichojifunza nilikuwa nikikiandika,ili baadaye ntakapojisahau nijue wapi pa kuanzia. Lakini nilijiahidi kuwa baada ya hapa,nitatoa vitabu vyangu vitakavyoweza kuwasaidia wanafunzi kama mimi.Unaweza ukaangalia vidio,au kusoma vitabu na usione matokeo yoyote .USIJALI UKO ENEO SALAMA.Baada ya masomo niliandika kitabu kinachoitwa OPEN THE DOORS OF SUCCESS IN YOUR ACADEMICS,kitabu hichi kina mbinu tisa ambazo naamini kabisa ztakutoa eneo ulilopo hadi eneo unalohitaji kuwa.
/AVvXsEgGVMH85m0xjK3TRpiPUcWY6yJg7Moik22hqOKOTmhMSzRURW2nISJEv3hd9tNciayAIsS2kYiftK45MCcSiMeDHeLh7tpoezUAvQN1ql5k1DTb2Kje8BIWjvD0A19FRgQc_OkLl0rafe_FS2Y3pwRoOCCCfiprU-MftfaxRQxYyuO-n9m8hsin3WT38g/s200/IMG_20221026_125457.jpg"/>
. Sasa ngoja tuende moja kwa moja kwenye hizo mbinu,usiwe na hofu,hakikisha una angalia hadi mwisho: 1.JITAMBUE WEWE BINAFSI. Kati ya vitu vnavyofanya mtu ashindwe kufanya vizuri kitaaluma ni kuwa wengi huwa hatujitambui.Kujitambua ni kufahamu|kujifahamu vizuri zaidi kitaaluma kuliko mtu mwingine yeyote. Kuna vitu ambavyo unapaswa binafsi kuvifahamu kama: >Fahamu ni vitu gani unavipenda >fanamu ni vitu gani huwa huvipendi >fahamu ni somo gani na mada gani unazoziweza kwenye masomo yako >fahamu ni somo gani na mada gani ambazo huwa znakushinda >fahamu mazingira unayopenda kusomea Kuvifahamu vitu,kama hvyo vitakuepusha kupoteza mda wako kwenye mambo yasiyokuhusu.Andika mahali kwa ajili ya kumbukumbu njema ya baadaye. 2.JITOE KUMTUMIKIA MUNGU. Hakuna jambo ambalo tunaweza kufanya sisi wanadamu bila MUNGU na tukafanikiwa,hvyo kuyaweka masomo yako kwake na kumkaBDHI KILA,basi amini utafanikiwa. Kujitoa kumtumikia MUNGU,siyo kwamba kila mda na mara zote unasali.Hapa namaanisha inakubidi kabla ya kuanza masomo yako unajikabidhi kwake kwanza.Hata kwenye maandiko yanasema mkono wa tajiri na aliye na ufahamu mara zote hutawala. Hakikisha unavyopambana,kusoma ndivyo unavyozidi kujiweka karibu na MUNGU zaidi.Juhudi zako ziwe sawasawa na namna unavyomtafuta MUNGU.Usitarajie kuwa husomi na kusoma kwa juhudi,uka faulu kuliko wenzio.Amini dini yako na pia muamini muumba wako. 3.NIDHAMU BINAFSI. Kuna baadhi ya vitu,unapaswa kuwa na nidhamu binafsi,mwanzoni nilijua nidhamu binafsi ni kusalimia ndugu jamaa,marafiki,kuvaa nguo za shule vizurilakini nidhamu binafsi ni muhimu sana,endapo kama unahitaji kubadili kiwango chako cha ufaulu. Nidhamu bunafsi ni kujifunza kuwa vile unavyohitaji uwe.Kuanza kuishi maisha yako,na sio maisha ya kutazama watu wengine.Kuwa wewe. Nidhamu binafsi kuijenga ni suala linalochukua mda,sio suala la siku.Kuwa na nidhamu binafsi huweza kuchukua hata wiki tatu hadi miezi.Ni kuandika vile unavyohitaji kuwa na viwango unapenda kufaulu,kisha kuviishi.Wanafunzi wengi huwa tuna malengo na mipango lakini kinachoturudisha nyuma ni kuamini na kuishi kama tulivyokuwa mwanzoni. Mfano unahitaji,uwe unasoma kila siku saa sita,wakati unafahamu hapo mwanzoni kwako ilikuwa ni vigumu.Fahamu kuwa huo ndo wakati utahitaji kuwa na nidhamu binafsi. 4.MIPANGO. Siku zote hakuna safari isiyokuwa na mwisho.Hivyo hata kwenye masomo yako unapoanza unahitaji kuwa na mipango itakayokuwezesha kufikia mwisho unaouhitaji.Mipango mingi tunayoipanga huwa ni juu zaidi ya viwango tulivyopo. Usipange mipango mingi,wakati unafahamu kuwa huna nidhamu binafsi ya kuifikia.Hakikisha mipango yako yote unaweza kuisimamia na kuikamilisha. 5.BADILISHA MTINDO WA MAISHA YAKO. Mtindo wako wa maisha unapaswa kuwa wa kipeke yako.Kuna kipindi,nilkuwa naona namna ambavyo huishi maisha ambayo siyo yao,ili waendane na watu wengne wakiamini kuwa watafanya vizuri.Baadhi ya vitu,havihitaji uviige bali ujifunze mbinu ambazo,wenzio wanazozitumia kukupita kitaaluma.KISHA FANYA MARA KUMI ZAIDI YA WAO. Nakumbuka nilishawahi kuandika hvyo,wenzangu waliokuwa wakifanya vizuri walikuwa wakifanya mijadala au discussion nyingi,wanafanya mitihani mingi mbali na ya mwalimu. Kuwafikia wao,ilinibidi niwe na mbinu za kitofauti zitakazoniwezesha kuwafikia wao.Nikaziandika kwenye daftari,ili nifahamu mbinu nitazotumia.Kusoma huwa ni kama safari yenye mashindano ndani yake,unahitajika kuwa na mbinu za kushindana na adui zako.Mbinu za kipekee. 6.MUDA. Huwa wanasema watu wote tumepewa masaa 24,lakini utofauti wa mafanikio huja kwenye suala la mda.Ukiangalia vizuri,watu wanaofanya vizuri wanatumia mda wao vzuri na mwingi kusoma wakATI MWINGINE hatufahamu. Pangilia mda wako vizuri,na kujua ni wakti gani wa kusoma somo gumu au rahisi na mada gani za kusoma.Kufahamu namna bora ya kupangilia hvyo vyote ni vyema ukasoma kitabu hiki cha OPEN THE DOORS OF SUCCESS IN YOUR ACADEMICS.Ni kitabu kilichoweza kutumia lugha nyepesi,ambayo hata mwanafunzi yoyote anaweza kuelewa. 7.AFYA. Hakuna mpango wowote unaoweza kuutimiza huku afya yako ni dhaifu.Ni vyema endapo kama,utaijali na kuipenda afya hako na kuhakikisha baadhi ya nyakat unakula matunda au mbogamboga. Usile chakula kingi,ambacho kitakufanya usinzie wakati wa kusoma kula kwa kiasi. 8.ONDOA HOFU. Neno mafanikio huwa sambamba na neno kufeli,ikiwa hujawahi kupata alama ambazo znakukatisha tamaa ,fahamu kuwa bado hujafanikiwa. Kuna baadhi ya mitihsni tunapitia na kufanya vibaya,tunadharaulika lakini kumbuka huo mtihani bado hujasema wewe ni nani.Unnaweza kubadilisha hzo namba na ukafanya vizuri zaidi.Siku zote kufeli,hutujengea shauku na hasira au hisia ambayo kupitia hiyo unaweza kufanya vizuri zaidi kuliko mwanzoni. 9.MARAFIKI WANAOKUZUNGUKA. Fahamu kuwa kila mtu anaufahamu wake,unaweza ukawa na rafiki anacheza sana kuliko wewe na bado akakupita darasani,ni kwamba yeye anautofauti wake wa kusoma au ana uwezo mkubwa wa kukariri na kuelewa vitu,hvyo ukijilinganisha naye utajikuta uko pale pale. kuwa na marafiki ambao mnaelewana,mna ndoto na malengo yanayoendana.HIIYOTE ITAKUSAIDIA KUWA KWENYE VIWANGO UNAVOVIHITAJI. Kitabu hiki unaweza pia kukipata kwa mfumo wa nakala laini,kwa gharama ya shilingi 4000 tu.Endapo kama utakihitaji Tuma 4000 kwenda kwenye namba yangu 0746650818 JINA UPENDO ERNEST KITUNDU.Kisha nitumie ujumbe wa meseji kuthibitisha muamala na utakipata kwa njia ya whatsapp au email. je,mbinu hizi zmekusaidia?Usiache kuwatumia na wenzio yaani kushare.Lakini pia maoni yako ni ya muhimu sana kwetu. Kitabu hiki kinapatikana pia kupitia dlbookstore.com

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.