Header Ads

Header ADS

Namna bora ya kuhifadhi hela kupitia 50!30!20 rule

Imekuwa ni changamoto sana kwa watu kufahamu,namna bora watakayoweza kuhifadh fedha zao.Tumekuwa tukijifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa namna wanavyozitumia na kuhifadhi fedha zao lakini mara nyingine hujikuta tukishindwa kufanya hivyo. Suala la kuhifadhi fedha vizuri huwa ni nidhamu binafsi anayokuwa nayo mtu,huwezi tu kufanya jambo hilo kwa haraka linahitaji mda.Ili tuweze kufikia ndoto zetu naa mipango yetu ya baadaye tunahitaji mbinu madhubuti za kuzzuwezesha tufike kule tunapopahitaji.50!30!20 rule imeweza kusaidia baadhi ya watu kufikia malengo yako waliyojiwekea.Tuone ni namna gani hiyo ambayo tunaweza kuhifadhi fedha zetu kupitia hii kanuni. *50% rule. Asilima hizi 50,huwa ni mahitaji.Yaani vitu vya muhimu vya kila siku unavyovihaji.Vitu hivi ni vile ambavyo huwezi kuishi au kuendelea mbele hadi viwepo.Vitu hivi hujumuisha,>maji >umeme >afya >kodi ya nyumba >manunuzi ya kila siku hapa naongelea masuala ya kula,sukari,chumvi,mafuta,unga,mchele na mengineyo mengi. Hivyo endapo kama kipato chako kwa mwezi au wiki ni laki moja(100,000) basi utachukua 50 ugawanye na 100 ambao ni kama 0.5 kisha utazidisha na kipato chako cha 100,000 ni kama 50,000.Ambapo kwa kila kipato chako itakubidi uwe unahifadhi 50,000,kwa matumizi ya kila siku. Tafakari kipato chako,kisha chukua 0.5 ya kipato chako.Hiyo hela ndio utakayoitumia au kuihifadhi kwa ajili ya mahitaji yako ya muhimu. *30% rule. Asilimia hizo hujumuisha vitu ambavyo unavihitaji ila havina ulazima sana,nikiwa na maana unaweza kuishi bila kuwa navyo.Mfano wa vitu hvyo ni kama,>nguo,>hobbies nikiwa na maana vitu unavyovipenda labda kwenda kuogelea kwenye swimming pool,kwenda kwenye sinema na mengineyo mengi. Hivyo vibainishe kwenye daftari lako,kisha angalia unapaswa kuhifadhi fedha kiasi gani kwa ajili ya vitu hvyo.Chukua 0.3 ya kipato chako kama ni 100,000 ambayo ukizidisha na 0.3 utapata 30,000.Hvyo kwa kila mshahara wako utatakiwa kuhifadhi 30,000 kwa mahitaji yasiyo ya lazima. *20%rule. Asilimia hizi huwa ni uwekezaji pia unaweza ukawa unazitumia kulipia madeni yako.Inawezekana ukawa na madeni mengi,hvyo hapa utahitajika kuyapunguza madeni yako kwa utaratibu,lakini pia kukuza na kuendeleza ndoto zako au biashara yako.Hvyo kwa kila mshahara ulionao itakubidi utoe 0.2 mbili mara kipato chako.Kisha utahifadhi kiasi hcho kwa ajili ya kulipia vitu.Inawezekana sio madeni tu,lakini pia kwa tatizo la dharura litakalokulazima kutoa kiasi fulani cha fedha. hvyo ni muhimu kuweka akiba hiyo.Jambo la kukumbuka ni kuwa asilimia hizi hutegemeana na kipato cha mtu,pamoja na namna anavyotumia fedha au matumizi yake.NI bora kama utafahamu mapema gharama za matumizi yako,ndipo utakapoweza kutumia kanuni hii. JE UJIFUNZA KITU ~USIACHE KUTOA MAONI YAKO HAPA.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.