Header Ads

Header ADS

Jisimamie kama kiongozi.

Kipindi nasoma,neno kiongozi lilikuwa na maana nyingi sana.Wengi husema kiongozi ni mtu mwenye maono,mtu mwenye uwezo wa kuongoza idadi kubwa ya watu.Lakini,pengine,ulishawahi kujiuliza kuwa unaweza kuwa wewe ni kiongozi. Wengi hufikiri,kiongozi ni mbunge,diwani,wajumbe na wengineo,huku tukusahau kuwa kila kitu huanzia nyumbani.Nyumbani ni sehemu ambayo unaweza kujifunza namna kiongozi anavyoyaendesha majukumu yake kama baba,mama,dada na kaka. Mbali na hayo yote,namna unavyoendesha maisha yako,ni ishara tosha ya kuwa utakuwa kiongozi wa namna gani,kibiashara,kielimu,kiuchumi,kifamilia.Pengine ni unavyoweza kuishi na watu waliokuzunguka hiyo ni ishara tosha ya namna utakavyokuja kuishi kizazi cha baadaye. Swali la kujiuliza,NI KUWA UNAONA NAMNA UNAVYOENDESHA MAISHA YAKO,UNASIFA ZA KUWA KIONGOZI BORA? Kuna baadhi ya vitendo,ambazo huwa tunazichukulia kawaida sana lakini vinaweza kutujengea tabia isiyokuwa njema. WEWE PIA NI KIONGOZI,MIMI PIA NI KIONGOZI.Utofauti ni kuwa kila mtu yupo kwenye eneo lake,fikiria kwa nafasi uliyonayo kwenye jamii au familia.Umeweza kufanya majukumu yako kama kiongozi,kwenye hilo eneo? Tabia ya kupuuzia baadhi ya vitu,na kukata tamaa mapema huwa na matokeo makubwa sana,kwetu kama viongozi kwenye suala la vizazi vyetu vya baadaye. Hivyo kipindi nasoma nilipata nafasi ya kusoma kitabu kinaitwa LEADING WITHOUT TEARS,kitabu hiki kilinisaidia mbali na masuala ya kimasomo lakini pia kilinipa mawazo mengi kuhusu kujisimamia kama kiongozi.Hii inakuepusha kuepuka kufanya mambo unayoweza kujuta kizazi cha mbeleni: 1.MAAMUZI. Kama ilvyokawaida kuwa kiongozi huwa ni maamuzi.Maamuzi yoyote unayoyafanya kwenye maisha yako,ndyo huwa yanaona machaguzi na nini kitakachotokea kipindi cha mbeleni.Suala la kiongozi kuwa na maamuzi sio lazima awe kiongozi wa serikalini,bali fikiria kuwa wote huwa kuna baadhi ya nyakati ngumu ambazo huwa kama ni kikwazo kwetu au znaweza kutukatisha tamaa,namna ya kutatua changamoto hiyo hutokana na maamuzi utakayoyafanya kwa wakati huo. Embu jiulize maswali yafuatayo: *Ni changamoto gani,ulishawahi kuipitia maishani mwako na namna gani uliweza kufanya maamuzi? Mara zote kiongozi mwenye maamuzi sahihi,huchukua mda kujibu afu kufanya maamuzi.Maamuzi ya kiongozi siku zote hayapaswi kuelemea upande mmoja ingawaje kuna baadhi ya maamuzi inabdi mmoja afurahi.mwingine aumie na wengine wasielewe ni kitu gani unachokifanya.KUBALINA NA YOTE. jambo la kuhakikisha ni kuwa unalilolifanya unaona lina tija kwako na kwa watu wengine wanaokuzunguka hata kama sio leo au kesho. NI AINA GANI YA MAAMUZI,HUWA UNAFANYA PINDI MAMABO YAKO YANAPOENDA VIBAYA? usisahau kutuachia ujumbe wako,ili watu wengi zaidi wajifunze kutoka kwako. 2.MAONO. Maono naweza kusema ni namna mtu anavyoonekana baada ya muda fulani.Na ili maono mtu aliyonayo yawe kweli anapaswa kuwa na mipango inayoweza kutimiza na awe na uwezo wa kuleta mabadiliko. Maono ya kweli,huwa hayaendeshwi na mtindo wa maisha tuliouzoea kila siku,bali inabdi tuone kuwa kweli hapa unaleta mabadiliko.Maono huwa yanasimamiwa kikamilifu. Kwenye kitabu hicho,mwandishi anaelezea umuhimu wa kushirikisha jamii na familia juu ya mipango \maono kiongozi aliyonayo,kukumbusha watu wako ni kwa nini,kitu fulani kinapaswa kukamilika. Kiongozi bila watu,hawezi kuitwa kiongozi.Chukulia watu wa familia yenu au watu waliokuzunguka kama ni watu wako.Ingawaje kuna watu huofia kufikia maono yao wAKIWAZA namna watu wao watakavyowaona. Moja kati ya umuhimu wa kushirikisha baadhi ya watu kwenye mipango yako,ni kuwa mnaweza kusaidiana kipindi utakachokuwa umekwama. Ni vyema kuwa makini na aina gani ya watu,tunahitaji tuwe sio kazini tu hata kwenye mambo tunayoyafanya. Mfano moja kati ya vitu alivyoviongelea mwanafilosofia ADAM SMITH,kuhusiana na suala la kuleta mabadiliko eneo lolote ni lazima kuwe na mgawanyo wa majukumu.Kuna baadhi ya vitu unahitaji watu wa kuvisimamia:Baba yupo kazini,basi mama anabidi aangalie familia,mazingira ya nyumbani. Maono ya kiongozi inabdi yawe sambamba na watu watakaomsaidia. 3.KUJIAMINI. Ni sifa ya ajabu sana kwani hapa inaelezea kuwa kiongozi wa kweli huwa anaamini maamuzi yake.Nikiwa na maana huwa hasikilizi watu.Hi hutokana na namna anvyohitaji kufanya mabadiliko.Tuchukulie mfano wa masuala ya kielimu,ili mtu aongeze ufaulu wake inabidi awe na marafiki zake anaoweza kuongozana nao kusoma. Huwa tunatofautiana sana,kwenye suala la uchaguzi wa watu.Kwenye kila chaguzi unaloliamua katika maisha yako liamini na ulisimamie,ulipiganie usisubri watu kuja kupambania ndoto zako wewe. Suala huwa ni moja lakini,watu huwa na mitazamo tofauti,amini wazo lako na chaguzi lako ili kujijengea ujasiri.Endapo kama usipojiamini kuna baadhi ya vitu utashindwa kuvifanya,na kujutia baadaye.Hata watu wasipoamini ndoto na maono yako,anza kuyaamini wewe wao wataamini baadaye. 4.UFUATILIAJI. Fikiria kichwani mwako,ni mipango gani uliyojiahidi kuitimiza lakini umeshindwa kutimiza ndani ya mda uliojiwekea.Hii yote ni kwa sababu huwa tunapoteza shauku kubwa sana,katika upande wa kufuatilia mambo yetu.Kitendo hiki,hujenga tabia ya kuupuzia baadhi ya mambo makubwa yenye manufaa maishani mwako. Kwa kila unachokipanga,hakikisha unakitimiza ili uweze kujiamini.

Maoni 1 :

Inaendeshwa na Blogger.