UTAJUAJE ANAKUPENDA?:FAHAMU MAMBO YATAKAYOKUSAIDIA KUWA NA MTU ANAYEKUPENDA.
Habari,ndugu zangu.Leo tutaona jinsi ya kujua unapendwa au unajipendekeza kwa mtu.
Katika maisha yetu ya kila siku,suala la Upendo ,ni jambo ambalo mbali na kutujenga hutufanya pia kuwa watu wa kufahamu mambo mengi.Lakini tatizo huja,wakati unapoumizwa na mtu uliyemwamini,rafiki,au hata jamaa zako.
Mara nyingi hujikuta,yule anayependa zaidi ndiye anayeumia,kwani anayempenda anaweza asiwe na mawazo au hisia tulizonazo juu yao.
Mahusiano mazuri huanza na urafiki.Sasa ili usiumie zaidi,hakikisha kwenye urafiki wenu,mwenzio anasifa zifuatazo zitakazokusaidia.Jambo ninalolifahamu kwamba ni vigumu sana kwa mtu kujifanyisha kuwa rafiki yako wa kweli.
Hivyo basi,usipoteze mda wako katika kulazimisha urafiki au mahusiano na mtu huyo,utajikuta ukiumia zaidi.Watu hao huwa na mahusiano ya kibinafsi.
Kupitia mambo haya hutakuwa na hofu wala wasiwasi,juu ya urafiki wenu.Endapo kama upo na mtu ambaye hana sifa hizi,basi mahusiano yenu bado.
Tukirejea kutoka kitabu kiitwacho GET ANYONE DO ANYTHING.
1.ANAKUKUBALI.
Moja kati ya mbinu rahisi kumtambua rafiki,ni kuona namna gani huwa anakukubali.Kuna baadhi ya nyakati,huwa unamwambia mtu jambo fulani,ila haoneshi kukubaliana na jambo hilo.Hapendi baadhi ya vitu kutoka kwako.
Jaribu kumwelezea kuhusu kitu cha muhimu kinachoendelea na uone endapo kama anaonesha kukubaliana na wewe.Ikiwa husikilizwi,kipindi cha urafiki wenu,usitarajie kusikilizwa kipindi mkiwa kwenye mahusiano yenu.
Mara nyingi,rafiki wa kweli hukusikiliza,na kuonesha kukubaliana na wewe.Endapo hatajambo ulilomwambia halikumbuki,fahamu kuwa bado hujapata rafiki sahihi kwako.
2.UAMINIFU.
Uaminifu huwa ni suala la muhimu kwenye mahusiano.Mwambie rafiki yako,kitu kuhusu mtu fulani na uone,endapo ulichokisema kitamfikia mhusika.Rafiki wa kweli hutambua thamani ya uaminifu katika mahusiano.
Hakikisha kabla hujamwambia jambo hilo mtu huyo,basi umepata ruhusa kutoka kwa mhusika ili iwe rahisi kwake kukuletea mrejesho huo.Raiki asiye wa kweli,huwa hawezi kukaa na kitu hicho bila kukisema.
3.MAFANIKIO.
Mtu yeyote anaweza kukupongeza,baada ya kutimiza jambo fulani muhimu.Lskini huwa ni vigumu kutambua,ikiwa ni kweli wamefurahi au kuna jambo nyuma ya furaha zao.
Baadhi ya watu tulionao huwa na wivu na ghadhabu,pindi utakapofanikiwa kwenye mambo fulani.Rafiki wa kweli,hujivunia mafanikio yako,hawezi kuwa na wivu wa mafsnikio yako.
Angalia endapo kama rafiki yako ataonekana mwenye habari nzuri au mbaya,hayo yote yatakusaidia kugundua.
Rafiki wa kweli hukumbusha,kuwa mafanikio yako ni kwa ajili ya watu wengine/fulani.Huona kuwa ni suala la kushukuru kufika hapo ulipo.
Rafiki wa kweli,hawezi kukuchonganisha na mtu au watu kutokana na mafanikio uliyonayo.
4.MKWELI.
Rafiki wa kweli huwa ni yule anayekuambia mambo usiyopenda kuambiwa.Huwa anakuambia mambo ya kweli kukuhusu,lakini mara zote umekuwa ni mtu wa kukimbia ukweli wako na kujificha.
Rafiki wa kweli anakuambia kuwa hapa hujafanya sawa.Na pengine anakurekebisha katik baadhi ya tabia zako,ili ufate mwenendo unaofaa.Husema hayo yote hata kama ukichukia,lakini ana uhakika wa kukusaidia.
5.HESHIMA.
Mwambie kuwa unashauku na jambo fulani,ambalo ni zuri na la muhimu,katika maisha yako,pengine ungependa kumwambia eneo la faragha mkiwa wawili.
Rafiki wa kweli hutoa mda wake kukusikiliza,hawezi kutangaza mambo mliyoyaongea mkiwa wawili.Huwa inauma sana,ikiwa umemwamini na kumwelezza mtu kitu ns yeye akaenda kukitangaza.
Inaonekana ni namna gani,hata mkiwa katika mahusiano,atakosa heshima kwako.Na pengine anaweza kukudhalilisha mbele za watu,bila kujali utaonaje au utajisikiaje.Kuliko kuwa na mtu wa hivyo,ni bora ukailinda heshima yako kwanza.Hakikisha kuwa anakuheshimu na kuheshimu hisia zako.
6.KUJITOA.
Swali la kujiuliza,JE YUPO TAYARI KUACHA MAMBO YAKE,ILI AKUPE FURAHA?JE ANAJITOLEA KATIKA BAADHI YA VITU KUKUPA FURAHA?
Watu wengi wa sasahuwa na mahusiano ya kibinafsi.Mara zote mnapoongea huwa anajiwaza yeye na kujifaidisha,hawezi kufanya jambo linalowezza kuwanufaishaa wote.
Katika suala la kusaidiana,yeye huwaza kujisaidia yeye na watu waliomzunguka,pengine hakuwazii wewe.
Hakiisha hata kwenye mipango,anahusianisha faida kati ya pande zote mbli yaani wewe na yeye.
MUHIMU:Ikiwa kati ya manne niliyoyaandika anayatimiza au kuyafanya basi utakuwa na rafiki mzuri.
HITIMISHO:Unaweza ukawa unatamani kujifunza mambo mengi kutoka kwenye vitabu,basi tumekuja na suluhisho.Ni kikundi cha whatsapp mabapo tutakuwa tunachambuwa vitabu mbalimbali na ukajifunza mengi,kuliko kufanya manunuzi ya bei kubwa za vitabu.Gharama ya kuchambua vitabu hvyo itakuwa ni shilingi 1000 tu kwa mwezi.Tutajifunza vitabu vingi na tutakuwepo na watuu mbalimbALI tutakaohakikisha unapata uchambuzi mzuri wa kitabu.
Vitabu hvyo vitachambuliwa kwa lugha ya kiswahili,vikiwemo GET ANYONE DO ANYTHING,THE TEN TIMES RULES,THE RARE FINDINDS na vingine vingi.Ili uweze kuwa mmoja wa watu au wanakikundi,utapaswa kutuma kiasi cha shilingi 1000,kwenda namba 0746650818 jina UPENDO KITUNDU,utatuma jina kamili na kisha utaunganishwa kwenye kikundi hcho.
Usisahau kucomment na kushare.
Congratulations God lead you to the Top
JibuFuta