Header Ads

Header ADS

Mafunzo 6 ya kujifunza kutoka kwenye kitabu cha RICH DAD,POOR DAD.

Habari,
Kwanza ningependa kutoa radhi kwa ambao walipata shida,kusoma masomo yaliyopita.Ila kwa sasa unaweza kuyapata na kusoma kwa njia zifuatazo:

>Kwenye blog yangu kupitia kompyuta yako ambapo utasoma masomo bila tatizo.
>Simu ambapo itakupasa utazame video moja au u download game(michezo),ambayo tunaamini itakusaidia.
>Kundi la whatsapp,masomo yote ni bure.

Tunaendelea mbele:
1.Wote tunahitaji elimu ya fedha.

Mwandishi anasema kuwa wanafunzi wengi wanamaliza shule bila ya ujuzi wa fedha.
Wanajifunza kutengeneza fedha,lakini hawana mawazo juu ya namna ya namna kutengeneza fedha kutoka katika fedha walizonazo au namna ya kuzitumia fedha zao.
Tunahitaji elimu ya fedha ili tuweze kuchunga fedha tulizonazo.

2.Tofauti kati ya tajiri na maskini.

Tajiri:
Huwa wanazitumia kama ifuatavyo:
-Mahitaji
-Uwekezaji
-Matakwa.
Maskini:
Huwa wanatumia kama ifuatavyo:
-Matakwa
-Mahitaji
–Uwekezaji.
Mwandishi anaonesha hiyo kuwa tofauti kati ya maskini na tajiri.

3.Badilika mwenyewe.
Kubali kuwa wewe ni tatizo badala ya kulaumu familia yako kwa kutokuwa matajiri. Utakapogundua kuwa wewe ni tatizo,mazingira yako yatabadilika.

4.Tumia akili au ujuzi wako kukuingizia kipato.
Mwandishi anatueleza kuwa tunapaswa kufundisha akili zetu,namna ya;
-Kutafuta fursa.
-Kujichanganya na watu wenye akili.
-Kutumia fedha.
-Unahitaji kujitoa juu ya kile unachokifanya.

5.Usichanganye fani yako na biashara yako.
Mwandishi anaeleza kwamba unafanya kazi kwanza kwa bosi wako,kisha ushuru wa serikali,na mwisho ni makato ya benki. Lakini usisahau kuongeza kipato chako.
Unahitaji kazi za kila siku,ili kuongeza kipato chako.

6.Tumia mahesabu kuweka fedha zako.
Mwandishi anatueleza kuwa mahesabu ni kitu cha muhimu,endapo unahitaji kufanikiwa.
Mali:Huwa inaongeza fedha kwenye mfuko wako. Matumizi:huondoa fedha kwenye mfuko wako.
Matajiri mara zote,uhakikisha matumizi yao hayazidi kipato,huku maskini wao matumizi yao huwa mengi Zaidi kuliko kipato chao.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.