Header Ads

Header ADS

Mambo ya kufanya kipindi ambacho una wazo la biashara,wakati huna mtaji.

Je ulishawahi kuwa na mpango wa kufanya biashara ila hela huna?
Yaani katika kila unalojaribu kutaka kufanya unajikuta hela ndo changamoto.
Nakumbuka kipindi nakaribia kuhitimu shule,nilikuwa na mipango ya biashara mingi na mizuri. Changamoto kubwa ilikuwa hususani kwenye fedha ya mtaji.

Hivyo nikafikiria nikope fedha,kisha nifanye kazi nitairejesha.
Baada ya kukopa fedha,ile na kufanya nilichotaka.Bahati mbaya ilikuwa nilipata hasara kubwa na baadaye fedha niliyobakiwa nayo ilikuwa kidogo sana.

Isingefaa kuanza kitu kipya.Hata nilipomwelezea mtu aliyenikopesha hakunielewa,alikuwa ni mtu wa kunilalamikia. Nilipitia kipindi kigumu,sikuwa Napata usingizi.Niliugulia maumivu ya ndani kwa ndani.
Watu niliotarajia wanifariji walipotea wote,nikabaki bila kitu.Baadhi ya nyakati,unalia lakini baadaye machozi yanaisha.

Hivyo nikaamua kutulia na kurudi upya,hali ya yote changamoto huwa zipo. Kuna baadhi ya vipindi huwa tuna mawazo mazuri sana,tena kipindi ambacho huna fedha.>br> Huwa tunakuwa na mipango ya kufanya mambo makubwa,lakini changamoto huja kwenye fedha.
Unaona kabisa,ili mambo yaende vizuri inahitajika fedha kuendesha huu mradi au wazo. Lakini ushauri ni upi TULIA.Namna moja au nyingine,neno kutulia huwa ni gumu sana kulikubali.

Ukifanya jambo hili,ukashindwa unaona uhamie na sehemu ingine.Na hiyo sehemu ingine nayo unashindwa. Mwisho wa siku unakuwa mtu wa kutapatapa.Huna jambo moja ulilolifanya,na ukajivunia umeliweza. Changamoto zinapojitokeza,wewe ndo mwisho wako.
Nilishawahi kupitia hiyo changamoto kubwa hivyo ninaposema inabidi UTULIE namaanisha. Sio mara zote matarajio yetu,huwa sawa sawa na uhalisia wa jambo.Ikiwa jambo lenyewe ndo upo hatua za mwanzoni.Hatua kama hii huwa ndipo ndoto na malengo yote huisha. Endapo kama mwanzo mzuri mwisho nao utakuwa ni mgumu.

Ulishawahi kuwa na wazo(mawazo) ya kufanya biashara,alafu ukawa unajiuliza:

>Sina mtaji?
>Sina ujasiri wa kwenda kuuza.
>Nitaonekanaje kama nikishindwa.
>Nitafanyaje wakati bado naonekana mdogo?
>Nitafanyaje huku hakuna anayenisaidia.
>Mbona kama hii kazi ni ngumu?
>Nitafanyaje huku bado ninasoma?
Wakati huo maswali haya,yalikuwa yananiumiza sana akili.Sikuwa na la kufanya. Mara zote nilionekana,mtu mwenye mawazo sana.
Hakuna kitu kigumu maishani kama kukubali umeshindwa.Hii huwa ni vigumu kwa watu kukubaliana na ukweli nimeshindwa na kuendelea mbele. Baadhi ya nyakati inabidi ukubaliane na matokeo.Ikiwa huna fedha ya kuanza nayo kama mtaji,fanya yafuatayo?

1.Ongea na familia yako.
Fahamu kuwa sio kila mtu anapaswa kufahamu unalohitaji kufanya. Unaweza kukatishwa tamaa na ukaacha mambo yako ya muhimu.Angalia ni nani kwenu huwa ni mrahisi sana kukusaidia,anakushauri na kuonesha jitihada za kukuwezesha kufikia malengo yako. 2.Jifunze mambo mbalimbali kuhusu jambo unalohitaji kulifanya. Kosa ambalo wengi wetu,tunafanya ni kuingia kwenye kazi bila kuwa na ujuzi mkubwa kwenye jambo husika. Hivyo hata,tukianguka kidogo tunashindwa kurudi tena kwenye viwango vikubwa. 3.Ongea na waalimu wako.
4.Tafuta mtu wa kukushauri.
5.Ongea na watu mbalimbali wanaofanya kazi kama yako.
6.Badilisha mipango yako.
Hayo yote utayapata kwenye kitabu cha KIPAJI KILETACHO MAFANIKIO.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.