Sheria 3 za fedha zisizofundishwa shuleni:Chukua hatua.
Hili ni moja kati ya somo nililofundishwa na nkajifunza,pia.Nmeona sio vibaya endapo kama tutajifunza wote.
1.Sheria ya kutengeneza fedha.
Sheria hii inasema ya kwamba UTALIPWA KULINGANA NA THAMANI UNAYOZALISHA,kwa maana kwamba ili kulipwa fedha ni lazima utoe thamani.
Ni lazima ufanye kitu ambacho kinawafaidisha wengine na wao wawe tayari kulipia kile ulichokifanya.
2.Sheria ya pili ni TUNZA FEDHA.
Kabla hatujaanza,Swali la kujiuliza,
Ukishapata fedha huwa unafanya nini?Umefanya biashara na ukapata faida,huwa unafanya nini?Au ukipokea mshahara,huwa unaufanyia nini?.
Watu wengi huwa wanakimbilia kutumia fedha ile waliyopata kwa kununua vitu ambavyo wanafikiri ni muhimu wakati sio muhimu.
Unajikuta unaona sehemu nyingi sana za kutumia fedha.Na kadiri unavyokuwa na fedha,ndivyo matumizi nayo yanaonekana.Kama kuna sehemu inayozalisha maskini wengi,ni kushindwa kutumia sheria hii ya pili ya fedha.
Kila unapopata fedha unasukumwa kuitumia,unaona vitu vizuri,matatizo ndivyo yanajitokeza na vitu vingine vingi.
Katika sheria hii,unahitaji kuweza kuitunza fedha,kuihifadhi kwa mda kabla hujafanya maamuzi yoyote.Hii ni hatua muhimu sana kama unataka kufikia mafanikio ya kifedha.
Hivyo,unapopata kipato chako,kabla hujakimbilia kufanya matumizi au hata uwekezaji,itunze kwanza kaa nayo,iweke kama akiba,japo kwa kipindi Fulani.
Halafu katika kipindi hiki ambacho unaitunza,endelea na maisha yako kama vile fedha ile haipo.Kwa mfano,kuna kitu unatamani sana kununua na ungeweza kununua kwa fedha uliyonayo,lakini unaamua kutonunua kwa sababu fedha hiyo ipo kwenye hatua ya kutunzwa.
Hata kama inakubidi kushinda njaa,fanya hivyo ,lakini fedha ile uwe umeitunza.Unaweza usielewe vizuri dhana hii ya kutunza fedha,lakini kwa kifupi ninachotaka ujenge hapa ni ile nidhamu ya wewe kuweza kuiendesha fedha na sio kuacha fedha ikuendeshe wewe.
Kwa sababu watu wengi wanapokuwa na fedha ni kama akili zao zinaacha kufanya kazi mpaka fedha ile iishe.Bila shaka umewahi kukutana na kauli hizi mimi nikipata fedha siwezi kutulia mpaka fedha hiyo iishe au ukiwa huna fedha unakuwa na mawazo mazuri sana,lakini ukishazipata mawazo yote yanapotea.
Yote haya yanatokana na kushindwa kuitunza fedha,kushindwa kuiendesha fedha na kukubali fedha ikuendeshe wewe. Tunashauriwa kutumia sheria hii ya fedha,pindi tunapopokea fedha au kipato chetu.Ukishatoa matumizi ya msingi,nyingine itunze na sahau kama una fedha umetunza.
3.Sheria ya tatu IFANYE FEDHA IKUZALISHIE.
Sheria hii nayo huwa tunafikiri tunaielewa na kuitumia lakini siyo kweli.Baada ya kupata fedha,kuweza kuitunza sasa unahitaji kuweza kuifanya fedha yako ikuzalishie.Hapa unaiweka fedha yako sehemu ambapo inazalisha faida Zaidi ya kipato unachopata sasa.
Kuna sehemu nyingi sana ambazo unaweza kuifanya fedha yako ikuzalishie Zaidi.Baadhi ya sehemu hizo ni:kuanzisha au kuendeleza biashara,hii ni njia nzuri kama una mda wa kutosha wa kusimamia fedha.
Sehemu zingine ni kuwekeza kwenye mali,vitu kama ardhi na majengo ambazo utazitumia kuingiza kipato:kuwekeza kwenye masoko ya fedha kama kununua hisa,vipande,na kadhalika.
Sehemu yoyote unayoweka fedha yako,hakikisha unapata faida.Kuna sehemu ambazo watu huwa wanafikiri wamewekeza,lakini ukweli ni wanapoteza fedha.
Baadhi ya sehemu hizo ni:kuweka fedha benki kwa kuamini unapata riba,hapo unapoteza fedha. Kununua vitu vya matumizi kama magari ya kutembelea,kuamini ukiwa na magari mengi ya kutembelea ni mali zinazokuzalishia,lakini ukweli ni hakuna kinachokuzalishwa kwenye magari mengi ya kutembelea,hasa kama hutumii yote kwenye kazi zako za uzalishaji.
Hizo ndio sheria tatu muhimu za fedha unazotakiwa kuzijua na kuishi nazo kila siku.Huenda ulikuwa unazitumia lakini ulikuwa unazitumia lakini ulikuwa hujazijua vizuri,sasa umeshazijua.Nakushauri uishi nazo na usijaribu kuvunja hata moja hapo,utajiingiza kwenye matatizo makubwa.Na maisha yako kuwa magumu.

Hakuna maoni