Mambo 7 yanayozuia mafanikio yako.
Habari,
Leo tutaenda kujifunza mambo 7 yanayozuia mafanikio yako
1.Tabia ya kujilinganisha na watu.
Kamwe usilinganishe mapambano yako ya maisha na ya mtu mwingine yeyote,na usikatishwe tamaa na mafanikio ya watu wengine.
Tengeneza njia yako mwenyewe katika mapambano yako kwa kujihamasisha na kutokukata tamaa.
Usisahau kuishi kulingana na kipato chako.
2.Tabia yako ya kutojiamini.
Kujiamini ni pale unapoamini kuwa una uwezo wa kipekee tofauti na mtu mwingine.
Unapojiamini unaupatia nguvu uwezo uliopo ndani yako ambao utakuwezesha kufanya mambo makubwa Zaidi katika maisha yako.
Ikiwa hutojiamini utazuia hali yako ya uthubutu wa kujaribu katika kufanya mambo kwa ajili ya mafanikio yako.
3.Marafiki wanaokuzunguka.
Mhenga mmoja aliwahi kusema
“Nioneshe rafiki yako name nitakuambia jinsi ulivyo”.
Akiwa na maana ya kuwa wewe ni mtu wa 5 katika idadi ya marafiki zako wa karibu wanaokuzunguka.
Ikiwa una marafiki 4 wavivu na wewe utakua mvivu wa 5.
Ikiwa una marafiki 4 wambea na wasengenyaji na wewe utakuwa mmbeya na msengenyaji wa 5.
Ikiwa una marafiki wa 4 walalamikaji na wewe utakuwa mlalamikaji wa 5.
4.Tabia yako ya kuishi bila malengo.
Uwezo wako wa kujiwekea malengo,ndio ustadi wako mkuu wa mafanikio yako.Malengo yako hufungua akili yako chanya na hutoa mawazo yenye nguvu kwa ajili ya kufikia malengo uliyojiwekea.
Ikiwa utaishi kwa malengo mafanikio yako yatapatikana hatua kwa hatua.
Na itakusaidia kuongeza umakini wako katika kila unachokifanya tena kwa kutokupoteza mda wako.
5.Tabia yako ya kuahirisha mambo.
Tabia yako ya kujisemea kuwa “Nitafanya kesho” Kwa kile ambacho ulipaswa ukifanye leo. Ni miongoni mwa mambo yanayozuia mafanikio yako.
Chochote unachotaka kukifanya,kifanye leo.Endapo kama kinawezekana kufanyika leo.
Kwa sababu,kesho unayoisubiri haitofika ina kesho yake pia.
6.Tabia yako kutokukubali kushindwa na kuchukulia kama mafunzo.
Unapojiandaa vya kutosha katika kila unachokifanya,ni lazima ujifunze kuwa kutakuwa na wakati utafanikiwa na kutakuwa na wakati utashindwa,nyakati zote hizi mbili ni muhimu.
Ikiwa wakati wa kushindwa utatokea basi,usikate tamaa bali utumie wakati huo kujifunza ni wapi umekosea na uanze upya.
7.Tabia yako ya kujidharau kwa kujiwazia mabaya.
Vile unavyofikiri na kuwaza ndivyo inavyokuwa au kutokea,hupaswi kujidharau kwa kujiwazia vibaya au kwa kuhofia maneno ya watu kupitia kile unachokifanya,au kushindwa kwako.
Amini kuwa wewe ni wa kipekee na una nguvu na uwezo mkubwa ndani yako uliopewa na muumbaji wako.
Hakuna mwingine kama wewe katika dunia hii na hatotokea.
Hili ni moja kati ya somo nililolipenda kwa Mwalimu Mkali Antidius.

Hakuna maoni