Header Ads

Header ADS

Kanuni za ubora:Zitakazokuwezesha kufanya mambo kwa ukubwa zaidi.

Hili ni somo linalofundishwa Golden edges group:
Chini ya Mwalimu Godlisten

1.Chagua na amua kuwa bora na kuboresha maeneo yako.
Mmoja ya walimu wazuri sana anaitwa John Maxwell aliwahi kusema

"Life is a matter of choices,and every choice you made makes you"
Ukweli ni kwamba sisi ni matokeo ya machaguzi tuliyowahi kuyafanya,na nyuma ya kila machaguzi kulikuwepo misukumo tofauti (marafiki,mazingira,hali,n.k)

Pamoja na ladha mbalimbali za hayo machaguzi ni muhimu kufahamu kuwa uchaguzi haufanywi na jamii,wewe ndiye mwajibikaji wa kwanza katika eneo la kufanya uchaguzi.

Chagua na amua kuwa bora.Muujiza wa uchaguzi ni kwamba baada ya wewe kuufanya uchaguzi,uchaguzi unakufanya wewe.

Chagua vyema.

2.Wekeza katika kujiboresha.
Hatua nyingine ya muhimu katika eneo lolote ambalo unasimamia ni kuwekeza katika kujiboresha kwanza.

. Ni muhimu ukubali kwamba wewe sio huduma,biashara,kazi wewe ni mtu.
Hvyo jipe nafasi ya kuwa na ukuaji binafsi katika eneo la maarifa na ujuzi.

"Gharama ya kuruhusu,huduma,kazi,biashara ikue kukuzidi wewe,ni kwamba itakuwa kubwa kuliko uwezo wako na hvyo baada ya muda hutaweza kuitawala na kwa sababu hiyo utaipoteza"

Kila mara jipe mda wa kujiboresha,usisahau tulijifunza awali dhana ya ubora ni katika eneo la watu na vitu.

Hivyo hakikisha vyote vinapata balance,ukuaji wako pamoja na kazi,huduma,biashara n.k.Weka uwiano ,weka balance.

4.Tengeneza mfumo.
Hivi umewahi kufikiri mwili wa binadamu uwe na vitu vyote kama ini,moyo,macho,na vingine vyote halafu usiwe na mifumo?
Naamini unafahamu kuwa mwili wako una mfumo wa chakula,mfumo wa kupokea na kutoa taarifa,mfumo wa kupokea chakula na kusambaza,mfumo wa kutoa taka.
Umewahi kufikiri mtu kaletwa na mwili hauna mfumo?Taka zinatokea popote ,hewa leo inatokea masikioni kesho puani ,umewahi kufikiri huyo mtu ataishi siku ngapi?

Sasa Mungu aliwaza ili mtu akue na aishi kufikia miaka 90 inabidi vitu vyote viwe organized,kuwe na mfumo.
Hakikisha chochote ambacho unataka kiwe na ubora,kipo organized ,kina mfumo.
Hapo namaanisha na wewe uwe na mfumo,jiwekee mfumo(mpangilio wa muda,mfumo wa fedha,namna ya kuhusiana na watu n.k)Jiwekee mfumo.

4.Tafuta na jenga mahusiano(mapya) na watu wanaofanya unachokifanya kwa namna bora sana.
Husiana na watu waliokutangulia kwa mtazamo wa kujifunza zaidi.
Kujifunza kwa kutazama pamoja na kunena nao.
Ujenzi wa mahusiano ya namna hii una lengo la;
*Kuamsha kiu/hamasa ya wewe kufanya zaidi.
*Ujenzi wa kimtazamo.
*Kuongea eneo lako la experience.
Hakikisha katika circle yako ya kimahusiano una watu waliokutangulia ambao unaweza kujifunza kwao. Imeletwa kwenu na
Upendo Kitundu
Mwandishi wa vitabu.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.