Header Ads

Header ADS

Mambo 5 muhimu ya kuzingatia pindi unapohitaji kuchukua mkopo:Elimu kidogo kuhusu mikopo.

Ningependa kubadilishana na wewe mawazo kuhusiana na mkopo.Labda sio wewe basi pengine ni mwenzako.Pengine labda sio leo ,ila kuna kipindi unaweza kuhitaji kukopa.
Hivyo leo kuna mambo 5 muhimu ya kuzingatia pindi unapohitaji mkopo au kukopa.

Ameandika Mr.Isaack Nsumba,nkaona sio mbaya kama na wewe utajifunza.;

1.Usikope fedha kabla hujajua kiasi vha riba unayopaswa kulipa.
Soma vizuri ujue riba ni kiasi gani na uone kama unaweza kuilipa au huwezi.Watu wengi likija suala la kukopa huwa wanakuwa na kimuhemuhe kiasi kwamba hawatulii ,kufikiria kwa kina.

2.Usikope fedha ili ukaanzishe biashara.
Kopa fedha ili kuendeleza biashara uliyoanzisha na ambayo imeanza kukuletea faida.
Na ukikopa nenda kawekeze fedha katika bidhaa zinazoleta fedha nyingi zaidi ya zingine,yaani zile zinazotoka mara kwa mara.

Hii itakusaidia kutengeneza faida nzuri kiasi cha kurudisha mkopo na riba yake.

. 3.Mikopo sio mibaya hasahasa ukiwa una elimu kuhusu mikopo na madeni inayoitwa "Loans and debts Management Education".
Mikopo ni moja ya income leveraging tool nikisema leveraging tool namaanisha kitu kinachokuza kipato.
Na inaitwa" Other people's money" na matajiri wengi wanajua namna ya kutumia hii.

4.Usikope fedha zaidi ya unayohitaji na usikope fedha kwa sababu tu una "access ya kukopa fedha".
Kama imebidi kukopa fedha lakini usikope zaidi ya ile unayoihitaji,kama unahitaji 3 milioni kopa hiyo na sio zaidi,ukikopa zaidi hiyo itakayozidi utaitumia vibaya.Na baadae itakuletea shida kubwa sana.

5.Usikope fedha ili kuingiza consuming properties,yaani mali zinazochukua fedha(liability).
Kopa na ukikopa fedha ipeleke kwenye income generating assets yaani vitu ambavyo kupitia hivyo vitakusaidia kutengeneza kipato.

Usikope fedha ili kununua TV,Simu,computers,Gari.Hivo vitaongeza matumizi yako ya fedha na baadae mkopo utakuelemea.
Mwisho;

Mikopo ni moja ya njia unayoweza itumia kupata mtaji fedha,na mkopo sio lazima uwe na riba.
Kama utakopa kwa ndugu,jamaa,na marafiki sidhani kama watakuwekea riba,ila ukikopa katika taasisi zozote zinazohusika na huduma za kifedha lazima kuwe na riba.

Japo riba zinatofautiana kati ya taasisi moja na nyingine ndio maana sometimes hata riba ya CRDB inatofautiana na NBC,NMB n.k
Na kiashiria kimojawapo kwamba una nafasi kubwa ya kufanikiwa kifedha ni uwezo wako wa KUKOPESHEKA.

Ukijiona hauwezi kukopesheka iwe na marafiki,ndugu na jamaa au taasisi za kifedha basi ujue una hali mbaya sana.

So,tengeneza mazingira watu waone fedha zao zikiwa kwako salama,ukifika hatua ya kuweza kupata mkopo iwe ni katika taasisi au kwa watu baki,basi jua una hali nzuri.
Imeletwa kwenu na Upendo Ernest Kitundu
Mwandishi wa vitabu,lakini pia nmejikita katika kutatua matatizo mbalimbali yanayoikumba jamii.
Mawasiliano yangu. Whatsapp: 0625734020
Namba ya kawaida:0746650818.Usiache kusoma vitabu vyaangu mbalimbali

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.