Header Ads

Header ADS

Maswali yatakayokuwezesha kugundua kipaji chako ambacho unaweza kukitumia na kujipatia mafanikio.

Moja kati ya maswali ambayo watu wengi hujiuliza ni kwamba,nitajuaje nina ujuzi fulani au kipaji ambacho watu wanaweza kunilipa kupitia hicho?
Suala la kugundua kipaji huwa ni gumu kwa baadhi ya watu ila siku zote kuna ujuzi fulani ambao unahisi kabisa nnao na nnaweza kupata mafanikio.Haya ni maswali baadhi unayoweza kujiuliza na ukaweza kugundua kipaji chako.

1.Ni jambo gani ambalo hupata msukumo wa ndani sana kulifanya?
Hili jambo huwa unalifanya mbali na kazi uliyonayo.

Nikupe mfano:Huyu mdada alikuwa famasia lakini mbali na hapo alikuwa anapenda kutengeneza keki.Na anapata msukumo wa ndani sana kuzitengeneza.

Fahamu kuwa unaweza kuutumia ujuzi wako na ukakusaidia kujiingizia kipato kizuri mno.

2.Jambo ambalo watu hupenda kujifunza kutoka kwako

Watu wanafahamu kuwa umebobea kwenye suala fulani hivyo watu hupenda kujifunza kutoka kwako

Mfano,Mama yangu ni mzuri sana kwenye suala la kutengeneza juisi.Na amekuwa akiziuza juisi hizo toka miaka na miaka.

Mbali na hayo watu walikuwa wakizinunua juisi kutoka kwake na sio mtu mwingine. 3.Jambo ambalo ikitokea hamna hela bado utalifanya?

Mara nyingi watu hufeli kwa sababu huweka fedha kama kipaumbele chao cha kwanza.
Unaweza kufanikiwa ikiwa kwenye huduma zako huifanyi fedha kama kipaumbele chako cha kwanza.

Lenga sana kwenye kutoa huduma nzuri kwa watu,kisha watu watakuamini na kukulipa kupitia ujuzi wako.

Kupitia maswali hayo,Je umeweza kugundua ujuzi au kipaji ulichonacho?Kwenye namna ya kukifanya kikupe mafanikio unaweza kukisoma kwenye link hii
https://www.getvalue.co/prod/kipaji_kiletacho_mafanikio

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.